Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Furaha yangu kuzinduliwa kesho Mwanza

11800 Kampeni+pic TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mwezi mmoja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua kampeni ya “Furaha yangu, Pima, Jitambue, Ishi’ jijini Dodoma kwa ngazi ya kitaifa sasa kampeni hiyo itazinduliwa kesho Julai 21 katika viwanja vya Furahisha jijini hapa kwa ngazi ya mkoa.

Akizindua kampeni hiyo jijini Dodoma Juni 19 mwaka huu, Majaliwa aliwaagiza wakuu wa mikoa nchini kushirikiana na wadau kufanya kampeni hiyo kwa miezi sita ili Watanzania wapate fursa ya kupima afya zao.

Wakati kampeni hiyo ikizinduliwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU)mkoani hapa yameongezeka na kufikia asilimia 7.2 kutoka asilimia kuanzia mwaka 2012 hadi 2017 kutokana na mwamko mdogo wa matumizi ya mipira ya kiume (kondomu).

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa  leo Julai 19, kuhusu uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa huo John Mongella aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupima na kutambua afya zao.

“Takwimu za mkoa wetu kufikia lengo la tisini tatu (90, 90, 90,) zinaonyesha kwa tisini ya kwanza ni asilimia 53 tu wanaofahamu hali zao, 90 ya pili, waliopimwa na kugundulika kuwa na VVU na kuanza kutumia dawa ni asilimia 74 na 90 ya tatu inaonyesha asilimia 72 tu walioanza kutumia dawa wamefanikiwa kufubaza virusi,” alisema Mongella.

Alisema takwimu hizo zinaonyesha idadi ya wanaopima wengi ni wanawake ni wengi kuliko wanaume hivyo kuwataka wanaume kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kampeni hiyo.

Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi Mkoa huo, Dk Pius Masele amesema Mkoa huo una watu zaidi ya 95,000 wanaosadikika kuwa na VVU lakini hawajitambui kama wameambukizwa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz