Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fundi magari apotea mazingira ya kutatanisha

Fundi Magari Apotea Mazingira Ya Kutatanisha Fundi magari apotea mazingira ya kutatanisha

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Issa Hamis Issa (44), Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga ambaye anajishughulisha na ufundi wa magari amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu novemba 2022 hadi sasa huku familia yake bila mafanikio.

Inadaiwa kuwa mara ya mwisho aliondoka nyumbani kwao Mkoani humo bila ndugu kujua ameelekea wapi.

Hussein Hamiss ambaye ni mdogo wa Issa alieleza namna ambavyo wamejitahidi kumtafuta ndugu yao bila kuwa na mafanikio yoyote mpaka sasa licha ya kutoa taarifa ya kupotea kwa ndugu yao.

Amesema tayari wametoa taarifa katika kituo Cha polisi Cha hapa Shinyanga na kupatiwa RB namba SHY/RB/5459/2022.

- Advertisement - “Tumejaribu kufuatilia baadhi ya vituo vya polisi kama hapa Shinyanga,Mwanza pamoja na Dodoma lakini kote wanatupa majibu kuwa hayupo wala hakuna taarifa yeyote inayomuhusu,”amesema

Naye, Saida Issa ambaye pia ni mdogo wa ndugu Issa anaishi Dodoma ameeleza kuwa familia imekuwa ikifanya jitihada kwenda kwenye vyombo mbalimbali vya Dola ili kusaidia ndugu yake kupatikana lakini hadi Sasa hawajapata matumaini yeyote na kuwaomba watanzania wenye taarifa kuhusu Issa kuisaidia familia ili impate ndugu yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live