Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fisi wawili wauawa, mmoja ana hirizi

Fisi Gt.jpeg Fisi wawili wauawa, mmoja ana hirizi

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Usimamiizi wa Wanyamapori (TAWA) wamefanikiwa kuwaua Fisi wawili walioripotiwa kupora Mtoto na kumjeruhi katika Kijiji cha Nsola Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ambapo Fisi mmoja amekutwa na hirizi mkiani (Kama inavyoonekana kwenye picha uki-swipe)

Afisa Uhusiano Mkuu TAWA, Vicky Kamata amenukuliwa akisema “Tarehe 24/4/2023 Ofisi ya Detach Mwanza ilipokea taarifa ya Fisi kupora Mtoto na kumjeruhi katika Wilaya ya Magu, Kata ya Nsola Kijiji cha Nsola ambapo Kikosi cha Askari watatu kilienda katika Kijiji hicho kudhibiti Fisi hao”

“Askari hao walifanikiwa kuwaua Fisi wawili na mmoja kati ya Fisi hao amekutwa na hirizi kwenye mkia kama inavyoonekana kwenye picha.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live