Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fisi watishia maisha ya wakazi Singida

11678 Fisi+pic TanzaniaWeb

Wed, 18 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Singida. Manispaa ya Mji wa Singida, imeanza kuwasaka na kuwaua kwa risasi fisi ambao wamekuwa tishio kwa wakazi hao.

Mpango huo unaosimamiwa na idara ya maliasili ya manispaa hiyo, tayari umefanikisha fisi wanne kuuawa baada ya kupigwa risasi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Lyapembile Kizito, alisema kuwa kutokana na msako huo fisi wawili walipigwa risasi na kufa papo hapo na wengine wawili kufia mbele ya safari baada ya kujeruhiwa vibaya.

“Fisi hao wanahatarisha usalama wa wananchi wanaowahi kazini alfajiri na wale wanaochelewa kurudi nyumbani usiku…juzi mfanyakazi wetu mmoja wa sekta ya usafi mjini alinusurika kushambuliwa,”amesema Bravo.

Alifafanua kuwa fisi hao wanasakwa kuanzia majira ya saa tatu usiku katika maeneo ya Mtaa wa Kindai ambao ndiyo hatari zaidi kwa usalama.

Baadhi ya wafanyakazi walionusurika kushambuliwa na fisi hao akiwamo Ester Saidi na Hassan Nyauli walipongeza zoezi hilo, kwa madai litawahakikishia usalama wa maisha yao wanapowahi kazini.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz