Geita. Watoto watano wamekufa baada ya kuliwa na fisi wilayani Nyang’wale Mkoa wa Geita tangu Januari 2020 akiwemo Nile Hassan mwenye umri wa miaka mitano.
Akizungumza leo Jumanne Machi 24, 2020 mkuu wa Wilaya hiyo, Hamimu Gwiyama amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kubainisha kuwa baadhi ya wananchi wamehamia kwenye maeneo ya milimani ambako ndiko kwenye fisi hao.
Amebainisha kuwa changamoto inayowakabili ni ukosefu wa wataalamu wa wanyamapori na kuwataka wananchi kutoshirikisha fisi na ushirikina.
“Sisi tumetoa taarifa mkoani kuomba watusaidie tupate ofisa wanyamapori ambao watawafukuza hawa fisi kutoka kwenye makazi ya watu warudi mlimani zaidi. Mara nyingi wananchi wenyewe wanaamua kuingia na kuwafukuza fisi ili kujiokoa,” amesema Gwiyama.
Diwani wa Shabaka, Mageni Mageni amesema katika kata hiyo watoto wanne wameliwa na fisi na kwamba wananchi wamechoka na hawatakuwa tayari kuvumilia.
“Nimepeleka kilio halmashauri kuomba ofisa wanyamapori aje huku ashirikiane na wananchi kuua fisi lakini hadi sasa hakuna aliyekuja na watu wanaendelea kupoteza watoto sasa tumesema basi tutawavamia hao fisi sisi wenyewe,” amesema.
Pia Soma
- Malawi kufanya uchaguzi wa marudio Julai 2
- Mtoto wa miaka 10 aozeshwa Tanzania
- Mbowe aeleza mwanae alivyougua ugonjwa wa corona
Robert aliwataka wananchi waliohamia kwenye maeneo ya pembezoni na milima kuhama na kurudi kwenye makazi yenye watu wengi ili kunusuru maisha yao.