Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fisi auwa watoto watatu

Fisi Aua Nguruew.jpeg Fisi auwa watoto watatu

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitongoji cha Gengeni kilichopo Kata ya Kambikatoto, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Mnyama Pori aina ya Fisi alivamia nyumba ya Shigela Ngasa [45] Mkazi wa Gengeni na kuwauwa kwa kuwang'ata watoto watatu wa familia hiyo ambao ni Samweli Shigela [05], Kasunzu Shigela [3] na Ngasa Shigela mwaka 1 wote wakazi wa Gengeni.

Aidha, katika tukio hilo mnyama huyo aliwajeruhi wazazi wa watoto hao ambao ni Shigela Ngasa [baba] na mke wake aitwaye Limi Masanja [38] wote wakazi wa Gengeni. Baada ya tukio hilo Fisi huyo aliua kondoo wawili na kisha akakimbia uelekeo wa Hifadhi ya Rungwa eneo la Kambikatoto.

Fisi huyo aliweza kuingia ndani ya nyumba hiyo kutokana na nyumba hiyo kutokuwa na mlango na iko porini karibu na Hifadhi hiyo. Majeruhi wamelazwa Hospitali ya Mtakatifu Gasper - Itigi, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa wanyama pori kutoka pori la akiba la Rungwa na Wananchi wa Gengeni limefanikiwa kumuua Fisi huyo ambaye alikimbilia Porini na baadae kurudi tena Kijini hapo.

Wakati huo huo, Mnamo Aprili O7, 2024 katika Kitongoji cha Katagho kilichopo Kiji cha Ngeleka, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, watoto watano walifariki dunia wakati wanapatiwa matibabu katika Zahanati ya Uhai Baptist baada ya kuzama ndani ya dimbwi la maji.

Watoto waliofariki katika tukio hilo wametambulika kwa majina ya Rahel Christopher Mwaikale [05] Mwanafunzi darasa la kwanza Shule ya Msingi Ngeleka, Carolina Anosisye Mwamkamba [kulwa] [06] Mwanafunzi darasa la kwanza Shule ya Msingi Makwale, Catherine Anosisye Mwamkamba [doto] [O6] Mwanafunzi darasa la kwanza Shule ya Msingi Makwale, Lightness Ephraim Kakenda [05].

Chanzo: www.tanzaniaweb.live