Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fedha za Covid-19 zaanza kutatua kero jimbo la Musoma Vijijini

WhatsApp Image 2021 10 25 At 11.46.56 AM.jpeg Fedha za Covid-19 zaanza kutatua kero jimbo la Musoma Vijijini

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: millardayo.com

Jimbo la Musoma Vijijini ambalo Mbunge wake ni Mhe Prof Sospeter Muhongo, limekuwa kinara wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Mafanikio ya Jimbo hili yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya Wanavijiji, Viongozi wao na Serikali yetu. Wanavijiji na viongozi wao, akiwemo Mbunge wa Jimbo, wamekubali kuchangia nguvukazi na fedha taslimu kwenye utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.

JIMBO la Musoma Vijijini limepata Tsh MILIONI 500 za COVID-19 kwa ajili ya kusambaza maji vijijini kufuatia mapendekezo ya Mhe Mbunge wa Jimbo.

MATUMIZI YA FEDHA hizo za COVID-19 ni kama ifuatavyo:

*Ujenzi wa TENKI la MAJI la mita za ujazo 200 (lita 200,000) Mlimani Nyaberango, Kijijini Nyambono.

*Usambazaji wa MABOMBA ya Maji kutoka kwenye TENKI hilo kwenda Vijiji vya KANDEREMA, BUGOJI na KABURABURA.

*Mlimani Nyaberango (Kijijini Nyambono) tayari lipo TENKI la MAJI (200 cu.m./lita 200,000) kwa ajili ya MAJI ya Vijiji vya SARAGANA, NYAMBONO na MIKUYU. Tenki hili limejengwa kwa kutumia Fedha za Bajeti za Mwaka 2019/2020

CHANZO CHA MAJI YA BOMBA YA VIJIJI HIVI SITA (6)

*Fedha za Bajeti ya Mwaka 2019/2020 na Mwaka 2020/2021 zimewezesha ujenzi wa MIUNDOMBINU ya kutumia Maji ya Ziwa Victoria kutoka kwenye chanzo kilichopo Kijijini Suguti.

*Maji ya kutoka Kijijini SUGUTI yanapelekwa hadi Kijijini CHIRORWE ambapo mabomba yametandazwa kupeleka maji Kijijini WANYERE na mengine kupeleka maji, kupitia Mlima Nyaberango, kwenda Vijijini SARAGANA, NYAMBONO na MIKUYU.

OMBI KWA WANAVIJIJI

*Wanavijiji wa vijiji vyote 6 wanaombwa kurahisisha upatikanaji wa maeneo ya kutandaza mabomba ya kusafirisha maji yatakayo kuwa kwenye MATENKI 2 Mlimani Nyaberango.

*Wanavijiji wanaombwa kuchangia NGUVUKAZI kuchimba mitaro ya kutandaza mabomba ya maji – tujitolee na tuchangie upatikanaji wa MAJI ya BOMBA Vijijini mwetu.

KUKAMILIKA KWA MRADI HUU

*Imepangwa kwamba, ifikapo tarehe 30 Disemba 2021, MAJI ya BOMBA yaanze kutumika ndani ya VIJIJI 6 vya: MIKUYU, NYAMBONO, SARAGANA, KANDEREMA, BUGOJI na KABURABURA.

SHUKRANI: *Shukrani za dhati zinatolewa na Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kwenda kwa SERIKALI YETU, na haswa kwa MHE RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MHE SAMIA SULUHU HASSAN, kwa kufanikisha upatikanaji wa FEDHA za COVID-19 na nyingine kwa manufaa ya TAIFA LETU.

PICHA za hapa zinaonesha:

*”Booster” iliyojengwa Kijijini Chirorwe kwa ajili ya kupandisha MAJI kwenda kwenye TENKI lilojengwa Mlimani Nyaberango, ndani ya Kijiji cha Nyambono.

*Tenki la Maji (Lita 200,000 – lenye ngazi pichani) ya Vijiji vya Saragana, Nyambono na Mikuyu lililojengwa Mlimani Nyaberango, Kijijini Nyambono

Chanzo: millardayo.com