Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia zilizobomolewa nyumba zahamishia makazi kwa RC

Familia Srst Familia zilizobomolewa nyumba zahamishia makazi kwa RC

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia 10 za Kijiji cha Mwasilimbi, Kata ya Ihusi Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, zimeweka kambi katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo baada ya kubomolewa kwa makazi yao.

Familia hizo zenye takribani watu 45, ambapo watu wazima ni 15 huku watoto wakiwa 30, zimefika katika ofisi ya mkuu wa mkoa jioni ya Agost 21, 2023 zikiwa na mahitaji matatu ya malazi, chakula na kufahamu hatma ya mgogoro huo wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 20.

Wakizungumza nasi kwa simu leo Jumatano Agosti 23, 2023 wawakilishi wa familia hizo wamesema wamekuwa wakilala kwenye ofisi hizo za mkuu wa mkoa kwa siku mbili tangu Jumatatu Agosti 21, 2023.

Wamefikia uamuzi huo baada ya makazi yao kubomolewa na mtu waliyedai walikuwa na mgogoro naye.

Mwananchi Digital lilijuzwa familia hizo zimekuwa zikilala hapo chini ya ulinzi wa polisi ambapo inaelezwa watoto hupelekwa kwenye moja ya ofisi ya majengo hayo huku wakubwa wakilala nje.

"Tumekuja hapa baada ya nyumba zetu kuvunjwa, hatuna nyumba za kuishi wala chakula kwasababu siku ambayo nyumba zilivunjwa tembo walipita na kula chakula tulichokuwa nacho na tunawatoto hatuna pa kwenda," amesema mwathirika mmoja ambaye jina tumelihifadhi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Simon Simalenga, alikiri kuwepo kwa mgogoro huo na mwenye eneo ambaye hakutaja, tangu 2002, na kwamba kilichotokea ni kile kilichoamriwa na mahakama.

“Hao watu walikuwa na mgogoro mtu mwingine ambao umedumu kwa miaka 20...tangu 2002. Mahakama ili rule out...wakashindwa kesi, kilichofanyika ni dalali wa mahakama kwenda kuvunja nyumba hizo. Na hii ni baada ya mdai kwenda mahakamani kuomba kukazia hukumu,” amesema na kuongeza;

“Mwaka 2017, wakati kesi ikiendelea, Serikali ya mkoa ya wakati huo, iliomba ilimsahawishi mdai kuwa kesi hiyo imalizwe nje ya mahakama jambo ambalo alikubali na akawa radhi kutoa sehemu ya eneo (heka 50) ili hawa watu waweze kupata eneo la makazi na kulima, na kipindi hicho zilikuwa familia kama 100, amesema Simalenga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live