Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia zenye watoto wa mazingira magumu wasaidiwa

1c4ac528af0aba05fb37636faa136eb9 Familia zenye watoto wa mazingira magumu wasaidiwa

Sat, 24 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mikumi Mission Church, lililopo mkoani Morogoro, kwa kushirikiana na Compassion Tanzania, limetoa msaada wa nyumba sita kwa familia zenye watoto manaoishi kwenye mazingira magumu.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, ambaye pia ni Askofu wa TAG, Jimbo la Morogoro Kusini, Peter Msimbe alisema lengo la kutoa misaada hiyo ni kuonesha upendo wa Kristo kwa jamii na kuinga mkono serikali katika kuihudumia jamii.

Alisema mbali ya kukabidhi misaada hiyo ya nyumba pia walikabidhi vitanda 29 na magodoro 29 kwa watoto wanaishi kwenye mazingira magumu.

Aliongeza kuwa Kanisa hilo kwa ushirika na Compassion wamelisaidia Kanisa la TAG Taifa kwenye eneo moja wapo la kipengele kilichopo kwenye mpango mkakati wa awamu ya pili ambacho ni cha uchumi na jamii.

Aliweka bayana kuwa TAG limeweka mkazo kwenye suala la kuanzisha miradi mbalimbali inayogusa jamii kwa upendo wa Kristo.

''Kwa hiyo sisi kama kanisa pamoja na washirika wenza wa Compassion Tanzania, tumeigusa jamii kwa kuwajengea nyumba watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Huduma hii tunaifanya bila ubaguzi wa kidini, siasa, kwa sababu upendo wa Mungu unagusa watu wote,” alisema Askofu Msimbe.

Alisema watu hawaliosaidiwa watakumbuka daima upendo wa Mungu na watakuwa sehemu ya kumpenda Kristo hata watakapokuwa watu wazima na mfano wa kuigwa kwenye jamii inayowazunguka.

Aliwaomba wazazi na walezi wajitahidi kuwalea watoto wao katika misingi ya Mungu maadili mema, ili wawe msaada kwao kwa siku za usoni.

Akizungumza kabla ya kukabidhi misaada hiyo, mgeni rasmi, Meneja Mwandamizi wa Shirika la Compassion Tanzania kutoka Makao Makuu jijini Arusha, Edwin Mugisha, aliitaka jamii kuwalea watoto katika maadili mema ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwa msaada kwa jamii.

Pia alisema nyumba hizo pamoja na madarasa yaliyojengwa hayatakuwa na maana kama wazazi watashindwa kuwalinda watoto wao na kuwafundisha uchaji Mungu.

Mmoja wa watoto waliopokea misaada hiyo alilishukuru kanisa la TAG kwa kushirikiana na Compassion kwa kuwakumbuka na kuwapatia misaada hiyo. Aliomba jamii na taasisi zingine kuona umuhimu wa kuwasaidia kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kutimiza malengo yao.

Chanzo: habarileo.co.tz