Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia: Nemes alisema atarudi Februari

Nemes Dsaf Nemes alisema atarudi Februari

Fri, 20 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia ya Mtanzania Nemes Raymond Tarimo (34) ambaye ameripotiwa kufariki wakati akipigana upande wa Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group dhidi ya Ukraine, imesema Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi umewaahidi kwamba leo Ijumaa Jan 20, 2023 utawapa taarifa ya lini mwili wa Kijana wao utaletwa Tanzania kwa ajili ya maziko.

Mjomba wa Nemes, Andrew Mwandenuka amesema aliongea na Nemes kwa mara ya mwisho November mwaka jana na alimuambia February mwaka huu atarudi Tanzania na baada ya hapo akapoteza mawasiliano nae hadi walipopata taarifa za kifo chake.

“Nemes ni Mtoto pekee kwenye Familia, Baba yake na Mama yake wote wamefariki, hii nyumba aliachiwa na Mama yake Mzazi na alipokuwa anarudi Tanzania alifikia hapa na alikuwa ni Mtu wa kujifungia ndani tu muda wote yupo na laptop yake, hakuwa na Marafiki wengi, hakuwahi kututambulisha Mke wala hakusema kuwa ana Mtoto.

“Tunachojua ni kwamba Nemes alikuwa Urusi anasoma hizi habari za kwamba alikuwa Mwanajeshi hatuzijui maana hakuwahi kuniambia kuwa na ndoto za kuwa Mwanajeshi, Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi umesema mwili wa Nemes utakapofikishwa hapa Tanzania atakuja Mtu na kutueleza ni nini kimempata Kijana wetu.

Jitihada za kuupata Ubalozi wa Tanzania katika Shirikisho la Urusi ili kupata taarifa za tukio hili hazijafanikiwa huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukisema unalifanyia kazi suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live