Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia 20 zakumbwa na mafuriko Kinondoni

Mafuriko Res Familia 20 zakumbwa na mafuriko Kinondoni

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia zaidi ya 20 katika mtaa wa Mkunguni A kata ya Hananasifu katika manispaa ya Kinondoni nyumba zao zimeingiliwa na maji kufuatia mvua iliyonyesha leo na hivyo kulazimu familia hizo kuishi maisha ya hofu kutokana na usalama wa maisha yao kuwa hatarini

Wakizungumza nasi, familia hizo zimesema hali hiyo imewasababishia kushindwa kutoka kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi na hivyo kutumia muda mwingi kuchota maji yaliyoingia ndani ya nyumba zao na kuyamwaga nje huku wakieleza vyombo pamoja na vitanda vimesombwa na maji

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Mkunguni A Jumanne Said ameiomba serikali kuharakisha zoezi la kuwalipa fidia wananchi hao kwani walishafanyiwa tathimini na kutakiwa kuondoka

Chanzo: www.tanzaniaweb.live