Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Extra Ordinary Men kutatua changamoto za Wanaume.

Gondwe Mkuu wa Wilaya Kinondoni Godwin Gondwe.

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia Idadi kubwa ya wanaume kukabiliwa na changamoto ya masuala ya afya ya uzazi, Jukwaa la Extra Ordinary Men kupitia Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Godwin Gondwe, amezindua jukwaa la Extra Ordnary Men na kuwataka wanaume kujitokeza kwa wingi katika kutatua changamoto zinazowakabili ili kuifanya jamii ya kinondoni kuwa salama.

Gondwe amewataka wanaume kutumia jukwaa hilo ili pia kuimarisha akili na nafasi ya mwanaume katika ngazi ya familia kama kichwa cha familia huku akisaidiwa na mwanamke.

"Tunasema kwamba mwanaume ndio kichwa cha familia, lakini katika familia mwanamke ndio shingo ya familia, kichwa hakiwezi kufanyakazi bila shingo, kwahiyo mwanamke pia ananguvu katika familia kuzidi mwanaume" alisema Gondwe.

Kwa upande wake Mratibu wa Jukwaa hilo Timothy Kyara amesema jukwaa hilo litawasaidia wanaume kutatua changamoto za afya na akili na hivyo kuwafanya wanaume kuweka wazi changamoto zao ili waweze kusaidika. "'Nafsi inasehemu tatu kuna akili,utashi, na uwezo wakufikiri lazima vyote vikae vizur, akili yako inapopata mawazo ambayo unashindwa kuyachakata vizuri ndio hapo sasa unaanza kupata shida, hisia zake zinaanza kurukaruka na kupelekea hasira muda wote, na ugomvi" alisema Kyara.

Jukwaa hilo la Extra Ordinary Men linalenga kuwakutanisha wanaume nchi nzima kwa lengo la kutatua changamoto mbali mbali za kiafya na kijamii. pia kuwajengea uwezo wa kueleza chanamoto zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live