Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Exim Bank Yatoa Zawadi ya Eid Kwa Watoto Yatima Dar, Mbeya, Shinyanga, Karatu

10.?fit=700%2C467&ssl=1 Exim Bank Yatoa Zawadi ya Eid Kwa Watoto Yatima Dar, Mbeya, Shinyanga, Karatu

Wed, 12 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Exim Bank Yatoa Zawadi ya Eid Kwa Watoto Yatima Dar, Mbeya, Shinyanga, Karatu May 11, 2021 by Global Publishers



Mkuuwa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim, Bw Stanley Kafu (Katikati) akikabidhi msaada ya vyakula na vinywaji kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanage kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam ili kuwawezeshawatoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani. Msaada wa aina hiyo pia ulitolewa na benki hiyo kwenye mikoa ya Mbeya, Shinyanga na Wilaya ya Karatu.

Dar es Salaam: Mei 11,2021; Benki ya Eximimetoa msaada wa vyakula na vinywaji kwenye vituo vinne  vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingiramagumu vya jijini Dar es Salaam, Mbeya, Shinyanga na Karatu  ikilenga kuwawezesha watoto hao waweze  kusherehekea vizuri sikukuu ya Eid El Fitr.



Mlezi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanahe Centre kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam, Bi Zamda Idrissa (wa pili kulia)akitoa neno la shukrani kwa benki ya Exim kufuatia msaada huo. Wanaoshuhudia nipamoja na Diwani wa Kata ya Makurumla, wilayani Ubungo, Bw. Bakari Kimwanga (wakwanza kulia)

Msaadahuo ulikabidhiwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo wakiwa wameambatana nawafanyakazi wengine na ulihusisha mahitaji muhimu ikiwemo mchele, mafuta yakupikia, sukari, unga wa sembe, unga wa ngano, maharage pamoja na katoni zajuisi na maji ya kunywa.



MenejaBenki ya Exim tawi la Mbeya Bi Shamsa Shambe (Kushoto) akikabidhi msaada yavyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Madina cha jijiniMbeya Bi Aisha Hamisi ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani

JijiniDar es Salaam, akiwasilisha msaada huo katika kituo cha kulelea watoto yatimana wanaoishi katika mazingira magumu cha New Faraja Orphanage Centre  kilichopo Mburahati jijini humo, MenejaMasoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu alisema imekuwa niutaratibu wa benki hiyo kusaidia makundi na taasisi mbalimbali kupitia ppangowake wa uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaofahamika kwa jina “Exim Cares”.



Meneja Benki ya Exim tawi la Mbeya, Bi Shamsa Shambe (Kulia) akikabidhi msaada yavyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru cha jijini Mbeya, Bi Mary Kassim ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.

“…Msaadahuu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, na ni mwendelezowa utaratibu wetu wa kile ambacho tumekuwa tukikifanya kila mwaka ambapowafanyakazi wa benki ya Exim pamoja na uongozi kwa ujumla tumekuwa tukiguswakuhakikisha kwamba watoto wanaoishi kwenye vituo hivi wanafurahia Sikukuu hizikama wenzao waliopo majumbani,” alisema.



Baadhi ya wafanyakazi benki ya Exim tawi la Mbeya wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bi Shamsa Shambe (wa pili kulia) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru cha jijini Mbeya mara baada ya kukabidhi msaada wa chakula ili kuwawezesha watotohao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.

BwKafu alivitaja vituo vingine ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja naKituo cha Watoto Yatima cha Nuru kilichopo jijini Mbeya, Kituo cha ShinyangaSociety for Orphans na kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija vilivyopomkoani Shinyanga pamoja na Kituo cha Shalom Orphanage and Children  Care Centre kilichopo wilayani Karatu.



Meneja Benki ya Exim tawi la Shinyanga Bi Sarah Tito (Kushoto) akikabidhi msaada yavyakula kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuuya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.

ZaidiBw Kafu alitoa wito kwa watoto hao kuhakikisha wanasoma kwa bidii hukuwakitanguliza nidhamu kwenye kila jambo wanalofanya ikiwemo masomo na shughulizao za kila siku wawapo shuleni na kituoni hapo.



Meneja Benki ya Exim tawi la Shinyanga, Bi Sarah Tito (wa tatu kulia) akizungumza wakati akikabidhi msaada ya vyakula kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans kilichopo Mkoani Shinyanga ili kuwawezesha watotohao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.

“Imekuwani furaha kwetu Benki ya Exim kuona kwamba tumekuwa tukipata wafanyakazi nawateja wenye mafanikio makubwa ambao baadhi yao wamepitia katika vituo hivi na kwasasawanafanya kazi zao kwa bidii na kwa weledi mkubwa. Ili hayo yatimie na kwenupia ni wajibu wenu kusoma kwa bidii pamoja na kutii maagizo ya walezi wenu kwanidhamu kubwa,’’ alisema.



Baadhi ya wafanyakazi benki ya Exim tawi laShinyanga wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bi Sarah Tito (katikati) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans kilichopo Mkoani Shinyanga mara baada yakukabidhi msaada wa chakula ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuuya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.

Kwaupande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru benki ya Exim kwa uamuziwake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuuya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine majumbani huku wakiomba taasisihiyo na wadau wengine kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbalizinazowakabili.



Baadhiya wafanyakazi benki ya Exim tawi laKaratu wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo, Bw John Ndyebonera (katikati) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Shalom Orphanage and Children Care Centre cha Wilayani Karatu wakati wakabidhi msaada wachakula ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kamawatoto wengine waliopo majumbani.

“Tunashukurusana benki ya Exim na wafanyakazi wote kwa kuguswa na kuona umuhimu wakuesherekea siku hii muhimu na watoto yatima. Tunaomba waendelee kuguswa iliwatusaidie zaidi katika kutatua changamoto nyingine ikiwemo suala la bima zaafya kwa watoto kwa kuwa baadhi yao hawana bima hizo muhimu.” alisema Bi ZamdaIdrissa Mlezi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja  kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.



Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim, Bi Mariam Mwapinga (Katikati) akikabidhi msaada ya vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanage kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha watoto hao wawezekufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Chanzo: globalpublishers.co.tz