Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ewura yatakiwa kuelimisha daladala

31905 Ewura+pc Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Kamati ya Ushauri ya Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura CCC) imetakiwa kuweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara na madereva na makondakta wa Daladala ili kuwaelimisha kuhusu wajibu na haki zao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema kundi ambalo lina changamoto nyingi na limekuwa likikosa mafunzo mbalimbali kwa kisingizio hawana muda wa kutosha hivyo kusababisha wakivunja sheria au kushindwa kujua wajibu wao kusingizia kukosa elimu ya kazi yao.

“Hili kundi limekuwa likisahaulika sana matokeo yake walio kwenye mnyororo huu kujikuta wako nyuma ya mambo kila mara na wengi wao wanapotakiwa kufuata sheria hudhani wanaonewa,” alisema Kamnda Bukombe wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa usafiri wa daladala jijini hapa jana.

Makamu Mwenyekiti wa muungano wa wenye Daladala jijini Tanga, Salim Al Mazrui alisema elimu waliyopata imewawezesha kujua wajibu wao katika kuihudumia jamii, pamoja na kupigania haki zao pale zinapokiukwa .



Chanzo: mwananchi.co.tz