Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Emmanuel ajiua kwa kujikata koromeo

Koromeo Weee Jeneza lililobeba mwili wa Emmanuel Roman

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Emmanuel Roman (51) mkazi wa kitongoji cha Sayuni, Kata ya Manyoni wilayani Manyoni mkoani Singida, amedaiwa kujiua baada ya kwa kujikata koromeo.

Emmanuel ambaye imeelezwa amekuwa akisumbuliwa na afya ya akili alikutwa amefariki nyumbani kwake jana asubuhi Desemba 10 ambapo kwa mujibu wa mashuhuda akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji hicho James Malyos wamesema walimkuta Emmanuel akiwa kwenye kochi huku mkono wa kushoto ukiwa na grinder lililosadikika kuwa alitumia kujikata huku kukiwa na jeraha Shingoni.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa, akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kutoa taarifa kamili ili kubaini hasa kiini cha tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live