Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Elimu nje ya mfumo rasmi iwanufaishe wengi'

'Elimu Nje Ya Mfumo Rasmi Iwanufaishe Wengi' 'Elimu nje ya mfumo rasmi iwanufaishe wengi'

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wito umetolewa kwa viongozi wa serikali, wataalam na maofisa elimu ya watu wazima kutafuta namna ya kutambua mahitaji ya wananchi mahali walipo, ili elimu nje ya mfumo rasmi inayotolewa iweze kuwanufaisha watu wengi zaidi.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu Msingi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Luoga alipokuwa anazindua Kituo cha Jamii cha Kujifunzia (Community Learning Center) kilichopo Ruvu JKT, Kata ya Mtambani, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.

Josephat amesema TAMISEMI wana dira ya elimu ambayo ina lengo la kuwa na Mtanzania aliyeelimika, mwenye maarifa, stadi na mtazamo chanya kwa ajili ya kujiletea maendeleo yake binafsi, jamii pamoja na Taifa.

"Jitihada za serikali katika kuendeleza dira hii imeweka mfumo wa elimu rasmi na elimu nje ya mfumo rasmi na kupitia elimu nje ya mfumo rasmi ndiyo tumewekeza kwenye vituo hivi, ili watu wazima ambao hawakupata elimu waweze kuipata kulingana na mazingira waliyopo," alieleza.

Aliitaka jamii iepuke watu wanaotoa tafsiri potofu kuhusu elimu ya watu wazima na waelewe kwamba elimu hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya sasa na baadaye.

Josephat alishukuru Shirika la DVV International kwa kuwajengea kituo cha kisasa ambacho kitawasaidia watu wa Kibaha Vijijini kupataeElimu nje ya mfumo rasmi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon amelishukuru Shirika la DVV International kwa kuwajengea kituo cha kisasa cha kutolea elimu ya watu wazima na kuwataka wananchi kukitumia kituo hicho ili kupata elimu zaidi.

"Mmi ni shabiki mkubwa wa kuboresha ubinadamu, moja ya njia ya kuboresha ubinadamu ni kujifunza kuandika na kusoma. Kujifunza tunaboresha mazuri ya ubinadamu wetu na tunadhibiti mabaya ya ubinadamu wetu," amesema Nickson.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live