Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Elimu jumuishi yaondoa unyanyapaa

1313400c8a8dc8c0c48a243b53666cc5.jpeg Elimu jumuishi yaondoa unyanyapaa

Thu, 10 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ELIMU jumuishi inayowashirikisha wanafunzi wenye ulemavu na wasio na ulemavu imesaidia kuondoa unyanyapaa kwenye jamii.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Kibaha Mjini, Happines Matagi, wakati akikabidhi viti mwendo kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani.

Matagi alisema kuwa kutokana na serikali kuweka mfumo wa elimu jumuishi umesaidia kuondoa unyanyapaa ndani ya jamii baada ya kupata uelewa na kuacha kuwanyanyapaa.

"Ni mafanikio makubwa sana kwetu kwani zamani watu wenye ulemavu walikuwa hawathaminiwi na walikuwa wakinyanyapaliwa na kuonekana kama watu wasiofaa ndani ya jamii, lakini kupitia elimu jumuishi imebadili dhana mbaya ya kuwatenga watu wenye ulemavu,"alisema.

Mshawishi na Mtetezi wa Shirikia lisilo la Kiserikali la ADD International linalosaidia watu wenye ulemavu, Asteria Gwajima, alisema shirika lao linashirikiana na serikali katika kutoa elimu na mafunzo kwa makundi yanayohusika na masuala ya watu wenye ulemavu.

Gwajima alisema wanatoa elimu kwa wanafunzi, walimu na jamii kuhusu namna ya kushirikiana na kuwatambua watu wenye ulemavu na ndiyo maana kumekuwa na mafanikio makubwa ndani ya jamii.

Chanzo: habarileo.co.tz