Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EWURA kanda ya ziwa yatoa msaada waandishi vifaa kujikinga na corona

WhatsApp Image 2020 05 13 At 3.jpeg EWURA kanda ya ziwa yatoa msaada waandishi vifaa kujikinga na corona

Wed, 13 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza wamepokea vifaa vya kujikinga na corona kutoka kwa Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji ( Ewura ) ili kuwanusuru na maambukizo wakati wakitekeleza majukumu yao.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Meneja wa Ewura Kanda ya Ziwa, George Mhina amesema waandishi wa habari ni kundi ambalo lipo kwenye hatari ya kupa maambukizo baada ya sekta ya afya hivyo baada ya kutambua umuhimu wameamua kutoa ndoo saba,vitakasa mikono 36, barakoa 100,tishu 200 na sabuni 12.

"Wasingekuwa waandishi wa habari tusingeweza kufahamu elimu ya corona na namna ya kujikinga leo kila mara tunapokea taarifa kupitia vyombo vya habari sekta hii ni muhimu sana" amesema Mhina

Naye Mwenyekiti wa chama hicho, Edwin Soko amesema waandishi ni watu muhimu hasa wakati huu kwa kuwa wanafanya kazi usiku na mchana kwa kufika popote kwa lengo la kuhabarisha jamii na kupata taarifa za mwenendo wa janaga la corona.

Amewaomba wadau mbalimbali kujitikeza kusaidia sekta hiyo ili wawe salama na jamii iendelee kupokea tarifa zenye tija na usahihi.

Katibu Msaidizi wa chama hicho, Blandina Aristides amewashukuru EWURA kwa kuguswa na kutoa msaada huo na kwamba utaongeza ufanisi katika kazi wakati wakitimiza wajibu wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live