Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Dunia inaweza kuzuia ndoa milioni 50 za utotoni’

22019 WATOTO+PIC TanzaniaWeb

Fri, 12 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Shirika la kimataifa la Save the Children limesema zaidi ya ndoa milioni 50 za utotoni zinaweza kuzuilika ifikapo mwaka 2030, iwapo wasichana watapewa nafasi ya kumaliza elimu ya sekondari.

Watetezi wa haki ya mtoto walisema, wasichana wanaoolewa wakiwa bado watoto hulazimika kuacha shule, kuwa na ukomo wa fursa za kiuchumi na kukabiliwa na hatari ya kuishi katika umasikini kuliko walioolewa baadaye.

Kwa mujibu wa mashirika ya utetezi, takribani wasichana milioni 15, wa kati ya umri wa miaka 15 na 19 wamelazimishwa kushiriki ngono, huku wasichana 7,000 wa kati ya miaka 15 na 24 wakiambukizwa Virusi vya Ukimwi kila wiki.

Inakadiriwa kuwa takribani wasichana milioni 10 wataolewa mwaka 2030 pekee na zaidi ya milioni 2 miongoni mwao watakuwa chini ya miaka 15.

Chanzo: mwananchi.co.tz