Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dugange atoa maagizo ujenzi wa barabara Njombe

DUGANGE Dugange atoa maagizo ujenzi wa barabara Njombe

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amemtaka mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara ya Igwachanya - Itulahumba yenye urefu wa kilometa 19.25 itakayogharimu Sh. Bilioni 9.86 kwa kiwango cha lami kuanza kazi kwa wakati na kuikamilisha katika muda uliopangwa kwenye mkataba.

Dkt Dugange ametoa agizo hilo wakati akishuhudia makabidhiano ya mkataba baina ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na mkandarasi kampuni ya Summer Communication Ltd itakayoanza kujengwa Desemba, 5 mwaka huu katika Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Claudia Kitta ametoa rai kwa mkandarasi wa mradi huo kutoa fursa ya ajira kwa wananchi wa eneo hilo badala ya kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo ya mbali.

Naye, Meneja wa TARURA Wilaya ya Wanging’ombe, Boniface Kasambo amesema mradi huo utakamilika ndani ya miezi 20 na kukamilika kwake kutarahisisha usafiri kwa abiria na mazao, kuimarisha kipato cha wananchi pamoja na kuifungua Wilaya hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live