Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dugange atoa maagizo ujenzi kituo cha afya Njombe

DUGANGE Dugange atoa maagizo ujenzi kituo cha afya Njombe

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Tamisemi, Dk Festo Dugange amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe kuhakikisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Ulembwe kukamilika ifikapo Desemba 30, mwaka huu.

Dk Dugange ametoa agizo hilo kwenye ziara yake ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kilipokea Sh462 milioni kwa ajili ya ujenzi huo.

"Nimepita kukagua ujenzi wa kituo hiki cha afya nimeridhishwa na ubora wa majengo, lakini kituo bado hakijakamilika na kilipaswa kukamilika Septemba mwaka huu lakini kwa sababu ya taratibu za kimanunuzi na mfumo kimechelewa, hivyo nimuagize Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha anasimamia ujenzi huu ukamilike Desemba 30 na Januari mosi, 2024 wananchi waanze kupata huduma,"

"Pili nataka nijiridhishe kwa sababu fedha iliyoletwa Sh462 milioni ilikua kukamilisha majengo yote na kwa sababu ujenzi umesimama, nataka nipate taarifa ya uhakika ndani ya saa 24 kama fedha iliyobaki inatosha kukamilisha majengo haya. Kwa lugha nyingine nisingependa kusikia kuwa fedha haitoshi kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan alileta fedha ili kukamilisha kituo hiki hivyo fedha zinapaswa zisimamiwe kwa weledi," amesema Dk Dugange.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live