Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dugange: Kibaha haikidhi viwango kuwa Manisipaa

Dkt. Festo Dugange Dugange: Kibaha haikidhi viwango kuwa Manisipaa

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema ilipokea wasilisho kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuchambua kwa kuzingatia vigezo vya kuupatia Mji wa Kibaha uliopo mkoani Pwani hadhi ya Manispaa ambapo haikukidhi vigezo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka aliyetaka kujua ni lini Serikali itaupatia Mji wa Kibaha hadhi ya Manispaa.

Serikali imesema ombi hilo kwa sasa lipo katika hatua za mwisho za uhakiki wa vigezo na mrejesho utatolewa kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live