Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma waagizwa kuongeza ufaulu

F13becd8971ad6ab0d29c20861ebcf65.png Dodoma waagizwa kuongeza ufaulu

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma, kuweka mikakati ya kuongea ufaulu.

Alitoa agizo hilo jana wakati akikagua ujenzi wa miundombinu ya Shule ya Msingi ya mfano ya Mtemi Mazengo jijini hapa. Alisema kuwa Dodoma ni moja ya mikoa inayosuasua katika katika ufaulu, hivyo lazima ziwepo jitihada thabiti za kuongeza ufaulu.

“Ufaulu katika mkoa huu uko chini sana ukilinganisha na mikoa mingine ambayo imekuwa ikibadilika kila mwaka kwa kuongeza kiwango cha ufaulu. Hivyo nendeni mkaweke mikakati na mbinu zitakazowasaidia kuongeza kasi ya ufaulu,” alisema.

Alisema Mkoa wa Dodoma una wajibu wa kuja na mbinu mbadala ambazo zitasaidia kuwafanya wanafunzi kusoma kwa bidi na kufaulu vizuri katika mitihani yao.

“Serikali imejenga miundombinu bora na kuweka mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia hivyo ni wajibu wa walimu kuhakikisha wanafunzi wanafaulu vizuri,”alisema.

Diwani wa Kata ya Ipagala, Doto Gombo aliahidi kuwa watahakikisha shule ya msingi Mtemi Mazengo inakuwa katika kumi bora mwakani, ili kuonyesha kuwa shule za serikali zikiboreshwa, zinaweza kufanya vizuri.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dk Suleiman Serera alisema mkoa umeweka mikakati ya kuongeza ufaulu na kuahidi kuwapo mabadiliko katika matokeo yajayo.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa shule hiyo, Mkurugenzi wa Jiji, Joseph Mafuru alisema halmashauri ilipokea Sh milioni 706 katika mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ya mfano.

“ Ili kuikamilisha, halmashauri iliongeza shilingi milioni 241.93, na sasa shule imesajiliwa kwa namba EM 18288 kwa jina la Shule ya Msingi Mtemi Mazengo” alisema Mafuru.

Alisema shule hiyo iliyokamilika Juni 29 mwaka huu, ilipangiwa walimu 21 na wanafunzi 660 wa Elimu ya Awali hadi darasa la sita, waliotoka kwenye shule tano za Ipagala B, Chadulu, Igahala, Mlimwa C na Medeli.

“Shule hii ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 725 ifikapo mwaka 2021 baada ya uandikishaji wa darasa la awali kukamilika mwezi Machi mwakani” alisema.

Kuhusu ufaulu, Mafuru alisema wanafunzi wa shule hiyo wameimarika kitaaluma na kuwa matokeo ya mitihani ya majaribio (mock) ya wilaya na mkoa, yanaonesha kuwapo kwa ongezeko za alama za juu na kuimarika kwa utunzaji wa mazingira, baada ya kupandwa miti 600.

“Halmashauri hii inatarajia kuwa na mafanikio makubwa ya kitaaluma kupitia shule hii ya mfano, kwani taarifa za awali zinaonyesha kuwa walimu wanajituma kwa kiasi kikubwa na matokeo ya majaribio na mitihani mbalimbali yanaonesha ufaulu wa juu” alisema Mafuru.

Chanzo: habarileo.co.tz