Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma kuwa Kitovu cha Kuzalisha Nyama na Maziwa

778b422373a054812838c6ca9eed650e Dodoma kuwa Kitovu cha Kuzalisha Nyama na Maziwa

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKOA wa Dodoma umeitaka serikali kuangalia namna ambavyo wataalamu wa afya ya mifugo waliopo katika ngazi za juu kuwa na utaratibu wa kufika katika maeneo ya chini ya wafugaji.

Amesema wataalumu wa ngazi ya juu wakifika maeneo ya chini kutaleta mkazo wa kutekeleza yale yote ambayo wataleta tija ya kuwa na mifugo mingi na bora.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Mukunda ambaye alisema “Wataalamu wa mifugo bado hawatoshi, hivyo ni vyema wataalamu waliopo katika ngazi za juu waweze kuwafikia pia wafugaji wa chini na tunataka kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kitovu cha kuzalisha nyama na maziwa kwa wingi.” alisema Mukunda

Alisema Sekta ya Mifugo kwa sasa imekuwa ikirasimishwa rasmi na kuifanya iheshimishe watu wanaofanya shughuli za mifugo kwa kuwa imekuwa na tija kubwa kwa taifa na mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Pauline Gekul amesema serikali bado inahakikisha inafanya jitihada mbalimbali za kupata masoko zaidi ya mazao ya mifugo yenye ubora ambayo yanachochewa na uwepo wa chanjo bora na mifugo kupatiwa chanjo hiyo kwa njia sahihi na pia kutoa angalizo kwa halmashauri nchini kuhakikisha zinakuwa na miundombinu bora kwa ajili ya kuogeshea mifugo.

“Wenzangu niwaombe popote huu waraka ulipo ukatusaidie ili malalamiko ya mnada umeharibika au wilaya nzima kutokuwa na josho, hayo malalamiko yafike mwisho kupitia mapato mbalimbali ambayo halmashauri wamekuwa wakipata yakiwemo ya minada iliyopo kwenye wilaya hizo, wanapaswa kutenga fedha kwa ajili ya kuyakarabati.” amesema Gekul

Chanzo: habarileo.co.tz