Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Waeleza jinsi fedha za UNDAP II zilivyosaidia

C5a813c76c4e7d93ab579d06ed3c3619 Dodoma Waeleza jinsi fedha za UNDAP II zilivyosaidia

Mon, 30 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MPANGO wa Pili wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania (UNDAP ll) ambao umekuwa ukifanyiwa kazi kuanzia Julai 2016 na mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini kwa kushirikiana na serikali ukiwa na bajeti ya Dola za Marekani bilioni 1.6 katika utekelezaji wake umefanikiwa kukusanya Dola za Marekani milioni 998.

Fedha hizo kwa mujibu wasemaji wa mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kamati ya majadiliano yaliyofanyika mjini hapa zimetumika katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kutekeleza malengo 12 ya maendeleo nchini Tanzania.

Katika mada zilizotolewa na Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Zlatan Milisic na Helge Flard, kiongozi wa timu inayosimamia utekelezaji wake zinaonesha kwamba fedha hizo zilitumika katika masuala ya kupambana na umaskini na ukuaji wa uchumi, haki za binadamu na usawa wa jinsia.

Pia imeelezwa katika mashauriano hayo kwamba kuna maendeleo yanayoonekana katika kusaidia miradi ya kiuchumi iliyiopangwa sawa na mpango wa maendeleo wa Taifa na Mkuza lll kwa upande wa Zanzibar.

Katika mkutano huo ambapo pia walikuwepo wawakilishi kutoka UNICEF, Shalini Bahuguna, mwakilishi Mkazi wa UNDP Christine Musisi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Tanzania Sarah Gordon.

Mambo manne yamefafanuliwa katika mpango wa UNDAP II ambapo mashirika 23 ya Umoja wa Mataifa yanashiriki kufikia malengo 12 ya maendeleo na mahitaji ya binadamu. Mambo hayo yanaamini kwamba ukuaji wa jumla wa kiuchumi unahitaji taifa lenye afya na linaloweza kuhimili majanga ya asili katika mazingira ya uwazi na utawala bora wakati wa kutoa huduma.

Katika utekelezaji wa UNDAP II, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanazingatia haki za binadamu, usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake, mazingira endelevu, utamaduni na maendeleo.

Mradi huo wa Bajeti ya Dola za Marekani bilioni 1.6 ulioundwa kabla ya Agenda 2030 ulitengenezwa kwa kuzingatia mahitaji ya mopango wa pili wa maendeleo na kuundwa kwa MKUZA III .

Pamoja na kufanyika kwa mkutano huo wa mashauriano, kamati ya pamoja ya serikali ya Tanzania na timu inaayoendesha UNDAPll walikutana kujadili juhudi za Tanzania katika kujiletea maendeleo na mafanikio ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Pia washiriki walijadili utekelezaji wa UNDAP II na mafanikio yake namna ambavyo pengo linazidi kuzibwa ili kusiwepo na mtu yoyote anayeachwa nyuma katika kufikia mafanikio ya kiuchumi na kijamii.

Katika dola za Marekani milioni 998 zilizokusanywa (Asilimia 50 ikiw ani ruzuku za maendeleo, asilimia 10 mikono na asilimia 40 misaada ya kibinadamu) ilibainika kwamba kuna changamoto kubwa ya kukusanya fedha kwa ajili ya mpango huo.

Katika majadiliano pande zinazohusika zilikubaliana kuongeza muda wa UNDAPll hadi Juni 2022 ili kuweza kusaidia mpango wa tatu wa maendeleo na MKUZA IV kuwa na mafanikio yaliyopangwa.

Kwa mwaka 2020/21 mipango ya maendeleo inatarajiwa kutumia Dola za Marekani milioni 296 huku masuala ya homa kali ya mapafu (covid-19) yakijumuishwa ndani yake kuangalia athari zake kwa jamii.

Pia kwa kushirikiana na serikali na sekta binafsi, imekuwa ikichagiza matumizi ya nishati mbadala, menejimenti ya uchafu na kuzuia ujangili wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania (UNDAP ll).

Aidha imeelezwa kuwa Umoja wa Mataifa na wadau wake wamekuwa wakishirikiana kuhakikisha kwamba watu wanajua kufanya menejimenti ya majanga na kupunguza athari zake katika kambi zinaoztunza wakimbizi kutoka Burundi, Kongo DRC wapatao 300,000 waliopo Kigoma Tanzania.

Ili kuimarisha masuala ya ulinzi na kupunguza vitendo viovu mipakani, Umoja wa Mataifa ulisaidia pikipiki zenye thamani ya Dola za Marekani 25,000 kwa idara ya uhamiaji ili kuiwezesha kuwa na uwezo wa kutoa msaada wa haraka kwa wakimbizi mipakani.

Katika mpango wa UNDAP ll akiwa na washirika 25 wamefanikiwa kutoa elimu na masuala ya afya kwa wakimbizi zaidi ya 280,000 wa Burundi na DRC na UN pia ilisaidia wakimbizi 22,110 wa Burundi kurejea makwao mwaka huu wa 2020.

Pia Umoja wa Mataifa hutoa chakula kwa wakimbizi 240,000.

Chanzo: habarileo.co.tz