Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa ukusanyaji wa mapato katika kituo cha Lusitu Wilayani Ludewa mkoani Njombe baada ya kugundua ubadhilifu wa mapato yaliyokusanywa.
Ametoa agizo wakati alipokutana na Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya pamoja na maafisa wa Uhifadhi na Maliasili Wilaya ya Ludewa na mkoa wa Njombe na kusema kuwa Wilaya hiyo inapaswa kukusanya zaidi ya shilingi Milioni 500 badala ya shilingi 47 iliyowasilihwa na Afisa Uhifadhi na Usimamizi wa Mistu, Bwana Ramadhan Said.
"Mapato yatokanayo na Misitu bado ni madogo, hii milioni 47 mliyokusanya hapa sijaridhika nayo, Misitu hapa ni mingi, Hapana hapa tunacheza" Amesema Dkt. Ndumbaro.
Aidha amesema ziara yake imelenga kuamsha uwekezaji katika sekta ya utalii ambayo imeonekana kutofanya vizuri licha ya kuwa na aina nyingi za utalii zikiwemo, mapango, wanyama, uoto wa asili, mali kale, hifadhi za taifa namaporomoko ya maji.