Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Cyril Chami kuzikwa Jumanne, Kibosho Moshi

A0a964d6fb0d67797fed16b998ec0547.jpeg Dkt. Cyril Chami kuzikwa Jumanne, Kibosho Moshi

Fri, 6 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWILI wa waziri wa zamani wa Serikali ya Tanzania, Dk. Cyril Chami utazikwa Jumanne ijayo Novemba 10, 2020 kijijini kwao Kibosho, Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

Dkt. Chami ambaye alizaliwa Februari 9, 1964, hadi hadi mauti yamkuta usiku wa kuamkia jana Alhamisi Novemba 5, 2020 katika hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma, alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Katika utawala wa awamu ya nne iliyoongozwa na Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete , Dkt. Chami alikuwa mbunge wa Moshi Vijijini-CCM na waziri wa viwanda na biashara.

Baada ya kuingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2005, aliteuliwa kuwa naibu waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Dkt. Chami aliangushwa Anthony Komu wa Chadema.

Mdogo wa Marehemu ambaye pia ndio msemaji wa familia amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu maeneo ya Nzuguni mkoani Dodoma na atasafirishwa kupelekwa Kibosho Moshi kwa mazishi.

“Tumepokea msiba kwa masikitiko na hatukuwa tunategemea ingetokea hili la kutokea, ni pigo kubwa kwa familia,lakini hatuna jinsi ni mapenzi ya Mungu, Jumatatu ijayo tutasafirisha mwili kwenda nyumbani Moshi kwa mazishi siku ya Jumanne,” amesema Steven.

Chanzo: habarileo.co.tz