Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Shein ahimiza uzalendo Mzumbe

B082019446b209c62472590716489756 Dk Shein ahimiza uzalendo Mzumbe

Wed, 27 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wafanyakazi wa chuo hicho kutanguliza uzalendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kukipaisha chuo hicho.

Dk Shein amebainisha hayo alipofika kujitambulisha katika ndaki ya chuo hicho iliyopo mkoani Dar es Salaam.

Amesema kuwa uzalendo na ushirikiano ndio utakipaisha chuo hicho kitu kitakachosaidia watu wengi kukimbilia hapo wanapotaka kuendeleza taaluma zao.

“Nasisitiza uzalendo kwa wafanyakazi wote pamoja na kuwa na ushirikiano kwani mipango ya chuo iliyopangwa haiwezi kutimia pasipo ushirikiano” amesema Dk Shein.

Chanzo: habarileo.co.tz