Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Ndumbaro apiga jeki misikiti nane Songea

Zulia Pic Data Dk Ndumbaro apiga jeki misikiti nane Songea

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea mjini, Dk Damas Ndumbaro ametoa msaada wa mazuria 180 kwa misikiti nane ya Manispaa ya Songea ili kuwaondolea changamoto ya ukosefu wa mazuria ya kusali.

Akikabidhi msaada huo Machi 20 kwa Jumuia ya Wanawake wa Kiislam (Juakita), Dk Ndumbaro amesema mazulia hayo yatawasaidia wanawake hao kumwabudu Mungu ambapo Misikiti nane ya   Majengo, Ruvuma, Lizabon, Mshangano , Msamala, Ndilima litembo ,Matogoro pamoja na Mjini  kila msikiti umepatiwa zuria 22 .

Amefafanua kuwa, awali alitoa zulia 27 kata ya mfaranyaki na ameshatoa tena  msaada wa mazuria hayo 180 hivyo anaamini yatasaidia waumini wa kislam kusali vizuri  na kuomba dua zitakazoleta neema mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla.

"Nimeona nikabidhi msaada huu kwa jumuia ya wanawake wa kislam baada ya kuridhishwa na uongozi wa Mwanamke  , Rais Samia Suluhu kwani ameliletea  heshima kubwa kwa wanawake wa Tanzania na taifa heshima kubwa duniani kwa kuweza kuleta maendeleo na kuongoza nchi kwa amani na utulivu,"alisema Dk Ndumbaro

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Juakita Mkoa wa Ruvuma, Mwajabu Kipande, amemshukuru Waziri Ndumbaro kwa msaada aliotoa amesema zulia hizo zinaenda kupunguza adha ambazo walikuwa wakipata waumini wa kislam hivyo zitaenda kuwafaa pia zimefika wakati muhafaka .

Amesema, wanawake wa kiislam wapo pamoja naye na wanamuunga mkono na kumuombea kwa Mungu afanikiwe katika shuguli zake pia waemuomba asichoke kuwasaidia kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Advertisement Meya wa Manispaa ya Songea, Michael Mbano amempongeza Ndumbaro kwa msaada aliotoa kwa waumini hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live