Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk. Nchimbi akabidhi rasmi ofisi kwa Dk. Mahenge

Kabdhi Ed Dk. Nchimbi akabidhi rasmi ofisi kwa Dk. Mahenge

Tue, 25 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo, Dk Nchimbi amemuomba Dk. Mahenge kutumia uzoefu aliotoka nao makao makuu ili kusaidia na kuivuta Singida kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa huo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo, Dk. Mahenge, amewaomba ushirikiano watumishi wa ofisi hiyo kama walivyokuwa wakimpatia mtangulizi wake ili kuwatumikia Wananchi wa Mkoa huo.

“Jamani ninawaomba sana ushirikiano wenu kama mlivyoona hapa mimi Mahenge nimeingia mimi kama mimi sijaja na wale niliokuwa nafanya nao kazi, nyinyi ndio wenzangu.” amesema Mahenge.

Aidha, Mahenge amewaomba watumie fursa hiyo kutafakari pale ambapo hawakufanya vizuri wakati wa Nchimbi kama ambavyo na yeye atatumia hiyo fursa kuongeza ufanisi wa utendaji wake wa kazi kama hakufanya vizuri wakati alipokuwa Dodoma.

Chanzo: ippmedia.com