Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mpango agusa tumbuatumbua kwenye mazishi ya Ndejembi

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

T: Dk Mpango agusa tumbuatumbua kwenye mazishi ya Ndejembi

 

S: Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Pacras Ndejembi aliyefariki Desemba 29, 2018 amezikwa Kitongozi cha Kizomoche leo jijini Dodoma.

 

-Ndejembi aliyezaliwa Novemba 30, 1929 amezikwa Kitongozi cha Kizomoche jijini Dodoma. Ameacha Mjane Leah, watoto 13, wajukuu 14 na vitukuu wanne.

 

Habel Chidawali, Mwanachi

[email protected]

Dodoma. Mambo mawili yameibuka leo Januari 1, 2019 katika msiba wa mwanasiasa mkongwe nchini Pacras Ndejembi baada viongozi kukumbushia tumbuatumbua ya viongozi.

Waziri wa Fedha na Mipango DK Philip Mpango amesema kitendo cha Ndejembi kudumu katika miaka 13 kwa ukuu wa wilaya ni jambo la kujifunza kwani viongozi wa sasa hawadumu hata miaka mitatu.

DK Mpango ambaye alikuwa akiiwakilisha Serikali amesema, hata katika kipindi cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere kulikuwa na tumbua ya watu wasiokuwa na maadili.

"Siku hizi sisi ukidumu miaka mitatu tu lazima umshukuru Mungu maana unaamka leo na kujikuta umetumbuliwa, huyu alidumu miaka 13 kwa kweli alistahili," amesema Dk Mpango.

Kwa upande wake Spika wa Bunge Job Ndugai amekumbusha misimamo ya mzee huyo ilikuwa ni pamoja na kumtoa aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Dodoma, Peter Mavunde. Mavunde ni baba mzazi wa mbunge wa Dodoma Mjini (CCM), Anthony Mavunde.

Ndugai amesema uamuzi huo ulikuwa mgumu kwa wakati huo lakini kwa sababu ya kusimamia haki iliwezekana.

Mtoto wa marehemu Edna Ndejembi amesema baba yao alitabiri kifo kwani aliwaita wajukuu wake akiwemo Deo Ndejembi (mkuu wa wilaya ya Kongwa) akawaambia mwishoni mwa mwaka wangekusanyika kwa furaha ‘ndicho kilichotokea’.

Kifo kisikie kwa mtu mwingine lakini kikikufika acha kabisa, pamoja na ukuu wa wilaya lakini Deo Ndejembi alishindwa kusoma historia ya marehemu babu yake alipojikuta akimwaga chozi.

Mbele ya umati wa umati wa watu tena wengi wakitoka Kongwa walishuhudia mkuu wa wilaya yao akishindwa kuzuia chozi lisimtoke.

Alikwenda mbele akionekana kujiamini na kuanza kusoma historia hiyo lakini alipofika kipengele cha ugonjwa akaanza kulia.

"Pole mheshimiwa, pole sana," alisikika mshereheshaji Mzee Peter Mavunde huku akitaka kumpokea kusoma lakini kwa kuwa ilibaki mistari michache alimalizia.



Chanzo: mwananchi.co.tz