Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Kimei amwaga TSh100 milioni Vunjo

Hewa Pic Data Dk Kimei amwaga TSh100 milioni Vunjo

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dk Charles Kimei ametoa msaada wa zaidi ya Sh100 milioni kwa ajili ya kusaidia miradi ya afya, elimu na maji kutokana na kata nyingi za jimbo hilo kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za kijamii.

Fedha hizo amezitoa kutoka katika akaunti yake binafsi kwa ajili ya kufanikisha miradi ya Elimu, Afya, Maji, Ulinzi, michezo na hazihusiki na fedha za mfuko wa jimbo.

Akizungumza katika kikao cha uwasilishwaji wa utekelezaji wa ilani ya uchanguzi Chama cha mapinduzi (CCM) ya kipindi cha mwaka mmoja 2020/21 Dk Kimei amesema lengo ni kuharakisha ukuaji wa maendeleo katika jimbo hilo.

"Nia na madhumuni ni kuhakikisha nasukuma maendeleo katika jimbo la Vunjo kwa kukamilisha ahadi zangu nilizoahidi kipindi niliomba kuchaguliwa na tayari nimeanza kutekeleza kwa vitendo kwa kutimia fedha zangu binafsi na nyingine kutoka serikalini" amesema Dk Kimei

Dk Kimei amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi zaidi ya  Sh2bilioni kwa ajili ya uboreshaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo barabara na maji.

Katika fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa jimbo la Vunjo limepokea kiasi cha Sh640 milioni kutoka mfuko wa Uviko-19

Advertisement Naye Mwenyekiti wa CCM Halmashauri ya Moshi Vijijini, Cyril Mushi amesema ni mbunge wa kwanza katika jimbo hilo kutumia mamilioni ya fedha zake binafsi kutekeleza miradi ya maendeleo.

"Huyu mbunge ni chaguo sahihi la wananchi wa Vunjo kwa kuwa sijawahi ona mbunge anatumia fedha zake binafsi kutekeleza miradi ya maendeleo chama kinaridhika na utendaji wa kazi zake za viwango"amesema Mushi

 Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Abbas Juma Kayanda amesema kwa namna mbunge anavyoshughulika na kero wananchi waendelee kumpatia ushirikiano ili kazi ya kujenga Vunjo iende kwa kasi.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz