Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema kutokana na kutofanyika kwa kazi ya kuandaa viongozi bora matunda ya kutoandaa vijana yameanza kuonekana.
Ameyasema hayo leo Alhamisi ya Mei 9, 2019 katika ibada ya mazishi ya Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Reginald Mengi inayofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini.
“Kuwa viongozi bora, watiifu, wanyenyekevu na wenye heshima, naomba nitumie fursa hii kumuombe msamaha kijana wangu Makonda mimi namfahamu na hii ni mara yangu ya pili namsema hadharani,”
“Mara yangu ya kwanza nilimsema Simiyu akaja analia ofisini nikasema ubadilike na kwa kweli ameanza kubadilika, bado ni kijana mzuri, shupavu lakini tunahitaji kuwasaidia vijana wetu,” amesema Dk Ally
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kitendo cha Dk Bashiru kuomba radhi kwa niaba yake ni upendo wa hali ya juu lakini alibainisha kuwa huenda trafsiri ya maneno aliyoyatoa hayakueleweka vizuri.
“Mimi niombe radhi kwa tafsiri hiyo kwa sababu nimemsifia mchaga katikati ya wachanga siyo mchaga katikati ya kabila lingine, mapokeo na nitaendelea kumuenzi mzee Mengi kwa mema yote aliyoyafanya kwa walemavu hasa katika mkoa wetu yatabaki kuwa alama,” amesema Makonda
Habari zinazohusiana na hii
- Mbowe akemea kauli za ubaguzi
- VIDEO: Mamia ya waombolezaji washiriki ibada mazishi ya Mengi
- Msafara wa Mengi wazuiwa saa moja kijijini
- VIDEO: Barabara zafungwa Moshi, wananchi wafurika kanisani ibada mazishi ya Mengi