Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Bagonza ataka uchunguzi wahalifu kuuawa na Polisi

Bagonzaa Dk Bagonza ataka uchunguzi wahalifu kuuawa na Polisi

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akizungumza kwenye mjadala wa kitaifa wa hali ya usalama nchini na operesheni mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Polisi ulioandaliwa na mtandao wa Watch Tanzania Dk Bagonza amesema suala la kufanyiwa uhalifu linaumiza lakini operesheni zinapofanyika na kuacha maswali inaumiza zaidi.

Amesema Ili kuondoa maswali kwenye jamii inahitajika suluhu ya pande zote kukubali uchunguzi Ili haki iweze kupatikana.

"Vyombo vyote vimeingiliwa vina baadhi ya watu ambao sio sahihi hata huku kwenye taasisi za dini wapo tusiteteane kwenye masuala yanayogusa uhai tukubali tusaidie Ili walioingia kwenye taasisi zetu wachukuliwe hatua,"amesema Bagonza.

"Wapo wanaopongeza na wanaolaumu tusijitetee tukubali kuchunguzwa," amesema.

Dk Bangonza alivitaka vyombo husika kufuata misingi ya haki na utawala wa sheria ili kuepuka wahalifu wanaojificha kwenye siasa, dini na familia.

Advertisement Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu  ameendelea kusisitiza kuwa waliuawa walikua wahalifu na kuwataka wananchi kuwapuuza wale wanaotetea uhalifu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime amesema operesheni zilizofanywa zimekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ushirikiano uliotolewa na wananchi.

Amezitaka familia, jamii na vyombo vya usalama kuwa na lugha moja ya kuzuia matukio ya uhalifu kwa kuwa suala la ulinzi sio la polisi peke yake bali la jamii kwa ujumla.

"Kwenye kukabiliana na uhalifu tusiwe na lugha ya kung'ata na kupuliza tuwe na lugha moja na familia turudi kwenye maadili kwa sasa familia zimeshindwa kusimama kwenye nafasi yake,"amesema.

Aidha amezitaka taasisi za dini kuongeza juhudi kwenye kufundishwa maadili na kuwataka viongozi wa mitaa na vijiji kusimamia ulinzi na usalama kwenye maeneo yao na kusema Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia haki na sheria ili kumaliza uhalifu kwenye jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live