TAASISI ya Dira Women Organization (DIWO) imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali wa Kikundi cha ‘TADAHA Women Products’ kilichopo Kibanda kwa Semkopi wilayani Muheza mkoani Tanga ili waweze kutengeneza bidhaa zenye ubora na viwango vinavyokubalika.
Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Taasisi ya Diwo ambao watawajengea uwezo wajasiriamali hao ili watumie ujuzi huo kujikomboa kiuchumi ikiwemo kutengeneza bidhaa ambazo zitakuwa na ubora mzuri.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mkurugenzi wa taasisi hiyo, Shamsa Danga alisema mafunzo hayo yatawawezesha wanawake hao kujengewa uwezo wa kuwa imara na kutumia fursa zilizopo ili kujipatia kipato.
Alisema, awali waliwakuta wajasiriamali hao wakitengeneza sabuni bila ya kupata mafunzo rasmi huku wakikabiliwa na vikwazo mbalimbali na ndipo walipoona wawapatie mafunzi ambayo yatayowawezesha kufanya shughuli za ujasiriamali wao kwa tija kubwa na mafanikio kuliko.
“Kikundi hiki tulipokutana nacho tuliwakutana na cheti lakini hakikuwa kinajulikana kisheria na nilitamani wajisajili ili waweze kujulikana.Cha kwanza niliwasaidia kusajili jina la kikundi chao cha TADAHA Women Products Brela na kusaidia alama za bidhaa za kibiashara (Barcode) ”Alisema Danga