Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani na mke wake wafariki kwa ajali Tabora

Diwani Ajali Na Mkewe.jpeg Diwani na mke wake wafariki kwa ajali Tabora

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diwani wa Kata ya Kalola wilayani Tabora (Uyui), Sauji Daud na mkewe, Magdalena Richard wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo Jumanne Oktoba 25, 2022.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Said Ntahondi amesema, diwani huyo na mkewe walikuwa katika gari yao binafsi wakitoka Kalola kuja Tabora mjini na ndipo gari lao lilipogongana na gari lingine uso kwa uso na wao kufariki papo hapo.

Amesema miili yao imepelekwa kuhifadhiwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete kwa ajili ya uchunguzi na taratibu zingine.

"Tunasubiri uchunguzi na taarifa nyingine za wana ndugu kabla ya kupanga mazishi yao," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live