Mabaki ya mwili wa Lighness Elia (29) aliyeuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa katika mashamba ya miwa ya TPC, bado yapo katika hospitali ya rufaa ya kanda ya KCMC, huku DNA ikisubirwa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa ili mabaki hayo yaweze kuhifadhiwa.
Wakati DNA ikisubiriwa bado jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kuwabaini waliohusika na mauajihayo, huku diwani wa kata hiyo ya Boma mbuzi Juma Raibu akiahidi shilingi milioni 5 kwa yeyote atakayesaidia jeshi polisi kukamatwa kwa watu hao.
Lightness Elia alikua mwalimu wa shule ya awali kata ya Pasua na ambaye alitoweka tangu tarehe 20 mwezi wa 7 na baadae mwili wake ulikuja kupatikana katika mashamba ya miwa ya TPC baada ya mbwa kuyavuta mabaki ya mwili wake pembezoni mwa njia.