Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani amkumbuka JPM ujenzi halmashauri

634a8551792194d64329f2ace1762fcc Diwani amkumbuka JPM ujenzi halmashauri

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

DIWANI wa Kata ya Suguti katika Halmashauri ya Wilaya Musoma, Denis Ekwabi amesema anaomboleza kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli huku akimkumbuka namna serikali yake ilivyoa Sh bilioni moja kuwezesha ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo katika kata anayoiongoza.

Alisema mchakato wa ujenzi wa makao makuu hayo ulikwama mwaka 2012 kwa kukosekana fedha, lakini umeanza na unatarajiwa kukamilika katika kipindi kisichozidi miezi sita.

Hata hivyo, kukamilishwa kwa mradi huo kutategemea utekelezaji wa serikali kwa kupeleka fedha nyingine kwa sababu ili mradi ukamilike, unakadiriwa kutumia Sh bilioni 2.7

Ekwabi alisema taarifa za kifo cha Magufuli zilimvunja moyo kiasi cha kukaribia kukata tamaa kwa kuwa aliamini uwepo uongozi Magufuli ulikuwa chachu ya maendeleo Musoma Vijjiji na maeneo mengine nchini, lakini Rais Samia Suluhu Hassan, amerejesha tumaini lake.

“Baada ya kupokea taarifa za kifo cha Magufuli, kwa kweli hali yangu ilienda mbali sana nikawa kama nimekosa matumaini, lakini kwa hotuba ya Rais Samia Suluhu, imenijenga upya,” alisema.

Akaongeza: “Mama (Rais) alisema vitu vingi sana akisisitiza yeye ndiye rais wa nchi; akasema watu wana mashaka kwamba huyu mwanamke ataweza, lakini akasema yeye ni mwanamke, ni kweli, lakini ndiye rais wa nchi… Kauli imenijenga upya.”

Alisema kauli hiyo iliyomkumbusha kuwa Rais Samia alifanya kazi na Magufuli tangu alipoingia madarakani na alimteua kuendelea kuwa makamu wake hata katika kipindi cha pili cha uongozi wake hali inayoashiria walirandana katika utendaji.

Ekwabi alisema anaamini imani Rais Magufuli kwa Samia, ilitokana na ukweli kwamba, anajua kila taratibu zilizokuwa zikifanyikaIkulu, hivyo ni dhahiri, atalifikisha taifa salama mahali lilipokusudiwa kufika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz