Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani aliyepotea akapatikana kwa Ashura, apotea tena, mke asema "Simtafuti tena"

DIWANI MPOTEVU Mke wa Diwani wa Kawe, Mutta Rwakatare

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa Diwani wa Kawe, Mutta Rwakatare, amekiri kutokujua ni wapi alipo mume wake huyo kwani hadi sasa unakaribia mwezi wa tatu bila diwani huyo kuonekana nyumbani na kusema amechoka na tabia hizo na hatohangaika tena kumtafuta.

Hayo ameyabainisha hii leo Novemba 17, 2022 na mke wa Mutta ambaye amesema kuwa awali alipopotea alikutwa kwenye moja ya gesti zilizopo wilayani Kinondoni akiwa na mwanamke na walifanikiwa kumrudisha nyumbani lakini baadaye alitoweka tena hadi leo.

Ikumbukwe awali diwani huyo alipotea ambapo taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilieleza kumpata akiwa nyumbani kwa Ashura maeneo ya Tabata Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live