Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani aliyekuwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji afariki

Diwani Afariki Diwani wa Buzilasoga wilayani Sengerema mkoani Mwanza (CCM), David Shilinde

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: Mwananchi

Diwani wa Buzilasoga wilayani Sengerema mkoani Mwanza (CCM), David Shilinde amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitari ya Rufaa ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza.

Shilinde ambaye alitumikia nafasi hiyo ya udiwani kwa tiketi ya CCM kwa miaka 13, alikuwa katika mahabusu ya Polisi kutokana na kutuhumiwa kuhusika kwenye mauaji ya Getruda Dotto, mauaji yaliyotokea Novemba 5,2022 kwenye Kitongiji cha Ikoni.

Kifo cha diwani huyo kimethibitishwa na mtoto wake, Fabian Shilinde ambaye ameieleza Mwananchi kuwa baba yake alifariki usiku wa kuamkia Jumatano, Septemba 27, mwaka huu akipatiwa matibabu hospitari ya Bugando.

Amesema kabla ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji, baba yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kisukari ambacho kwa mujibu wa madaktari ndicho kimepelekea kifo chake.

Chanzo: Mwananchi