Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani aliyekutwa kwa Ashura arejea kikaoni

DIWANI MPOTEVU Diwani ‘aliyepotea’

Fri, 24 Jun 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Hatimaye Diwani wa Kata ya Kawe, Mutta Rwakatare ameonekana kwa mara ya kwanza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Manispaa ya Kinondoni, tangu Meya wa Baraza hilo, Songoro Mnyonge alipotangaza kutoonekana katika vikao mbalimbali tangu Machi mwaka huu.

Mapema leo Juni 24, 2022, akitangaza kwa furaha na bashasha katika Baraza la Madiwani lililohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Meya Songoro Mnyonge, amesema diwani huyo wa kata ya Kawe ameonekana kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza kutokuonekana kwake kwenye mabaraza yaliyopita.

" .... baadae leo jioni tutakuwa na Get Together' na madiwani wengine kufurahia kurejea kwake, tunaamini hatapotea tena," amesema Meya huyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz