Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani ahoji kata kuitwa Zuzu, ataka iitwe Zinje

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi  amesema wanatarajia kuanzia mchakato wa kubadilisha jina la kata ya Zuzu na kuiita Zinje.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Julai 31, 2019 wakati kujibu swali la diwani wa Zuzu,  Awadhi Abdullah katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwenye baraza la madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dodoma.

Katika swali lake Awadhi alitaka kujua sababu za kata hiyo kuitwa Zuzu, nani aliyependekeza jina hilo na kwa sababu gani.

Katika majibu yake Kunambi amesema ni ngumu kujua nani aliyesema kata hiyo iitwe Zuzu pamoja na sababu za kuitwa jina hilo.

Amesema wamepokea mapendekezo kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo waziri mkuu wa zamani, Mizengo Pinda kuwa jina hilo lina tafsiri mbaya.

"Kwa kuwa si mstaafu tutaanza mchakato mara moja wa kubadilisha jina hili ambalo kweli tafsiri yake si nzuri ili tuiite  kata hii Zinje," amesema Kunambi.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz