Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani afariki ghafla Bunda

Diwani Diwani Kifo.png Diwani afariki ghafla Bunda

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

wani wa Kisorya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Amos Ndaro amefariki dunia.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Charles Manumbu amethibitisha kutokea kwa kifo hicho usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2024.

Manumbu amesema kifo cha diwani huyo ni cha ghafla, kwani hadi jana hakuwa na tatizo lolote la kiafya.

"Nimeongea naye jana, kuna mambo alitaka ufafanuzi lakini pia alikuwa na vikao kwenye kata yake ambavyo alivifanya hadi mwisho. Ninachoweza kusema mwenzetu amelala na Mungu ndiye anapanga saa ya kumchukua mja wake" amesema.

Amesema mwili wa marehemu umepelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi na kwamba baada ya uchunguzi watajua kwa undani chanzo cha kifo hicho na taratibu za mazishi.

"Nipo njiani naelekea huko, nadhani nikifika nitajua chanzo ni nini maana mwili tayari umepelekwa hospitalini kwa uchunguzi. Nimepokea taarifa za kifo saa 10.45 alfajiri na nimeambia amefariki nyumbani saa 9," amesema.

Diwani wa Kibara katika halmashauri hiyo, Mtamwega Mgahwa amesema taarifa za awali zinadai diwani huyo amefariki dunia kwa tatizo la shinikizo la damu.

"Ameugua ghafla usiku na kufariki dunia usiku huo huo, lakini jana kutwa nzima alikuwa mzima na aliendelea na shughuli zake kama kawaida,"amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live