Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva wa mwendokasi adaiwa kuwapitiliza vituo abiria kwa hasira

Kimara Mwendokasiii Mwendokasiiiii Dereva wa mwendokasi adaiwa kuwapitiliza vituo abiria kwa hasira

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dereva wa Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi) ambaye jina lake halijafahamika, akiendesha kutoka kituo cha Gerezani kwenda Kimara, amedaiwa kutosimama kwenye vituo vingi vya njiani baada ya kurushiana maneno na Abiria ambao walilalamikia uendeshaji wake.

Abiria mmoja amedai licha ya Basi kujaa, Dereva aliendelea kupakia abiria ambapo walilalamika kuwa anawaumiza kwa kufungua na kufunga milango, hali iliyoibua ubishani.

Baada ya kutoka Kituo cha Magomeni Dereva hakusimama, akawapeleka abiria wote Kituo cha Kimara Mwisho.

Anadai walipofika Kimara, Dereva alishuka na kuondoka na baada ya mvutano wa muda mrefu, Dereva mwingine akaamua kuchukua basi husika na kuwarejesha wale waliopitilizwa vituo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live