Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva wa lori aliyekimbia akutwa gesti

Mkama Rpc Ed 0 kamanda Mkama.

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika Operesheni za usalama barabarani zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Operesheni hizo zimefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 10 wa makosa ya usalama barabarani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kumkamata Samson Uwiringiyimana (35) Raia wa Nchi ya Rwanda ambaye ni dereva wa Lori aliyehusika katika tukio la ajali iliyosababisha vifo vya watu Saba na wengine Sita kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea Mei 14 mwaka huu maeneo ya Dakawa wilayani Mvomero mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 16 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Alex Mkama ameeleza mtuhumiwa huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni(Guest House) iliyopo Dumila wilayani Kilosa mkoani humo alipokuwa amejificha.

Aidha, Watuhumiwa wengine Tisa wamekamatwa kwa makosa ya kuendesha magari ya masafa marefu na magari ya abiria wakiwa wamelewa na kupelekea Leseni zao kufungiwa na kutakiwa kurudi katika vyuo vya mafunzo ya udereva kujifunza zaidi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewataka madereva wote kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live