Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva wa basi la shule amgonga mwanafunzi, amuua

Ajalii Shule Mfano wa basi la shule

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia dereva wa gari la shule ya Msingi Samuu, Kassim Said Mahona (40) kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa shule hiyo Godlight Chisawilo (04) kwa kumgonga na gari la shule hiyo Mjini Shinyanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando, tukio hilo limetokea Jumanne Juni 21,2022 majira ya saa 12 jioni katika maeneo ya Majengo Mapya Manispaa ya Shinyanga.

“Gari lenye namba za usajili T.151 DAG Toyota Coastar mali ya Malatia wa Shinyanga likitokea shule ya msingi Samuu kuelekea Majengo Mapya likiendeshwa na dereva aitwaye Kassim Said Mahona (40) na mkazi wa Nguzo Nane Shinyanga, lilimgonga mtembea kwa miguu Godlight Chisawilo (04) mwanafunzi wa shule ya chekechea Samuu na kumsababisha kifo chake,” ameeleza Kamanda Kyando.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara na tayari mtuhumiwa amekamatwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live