Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Nelson Rwangaza (43) mkazi wa Kamachumu aliyekuwa akiendesha gari la Shule ya Kemebos lililokuwa limebeba wanafunzi 35 na watumishi wanne wa shule hiyo na kuanguka katika Kijiji cha Kizilamuyaga, Kata ya Kimwani wilayani Muleba saa 8.30 usiku wa kuamkia Machi 24 mwaka huu na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na majeruhi wanne.
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Nelson Rwangaza (43) mkazi wa Kamachumu aliyekuwa akiendesha gari la Shule ya Kemebos lililokuwa limebeba wanafunzi 35 na watumishi wanne wa shule hiyo na kuanguka katika Kijiji cha Kizilamuyaga, Kata ya Kimwani wilayani Muleba saa 8.30 usiku wa kuamkia Machi 24 mwaka huu na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na majeruhi wanne. Katika hatua nyingine Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kuwa wamiliki wa shule hiyo walikiuka kanuni na taratibu za kuanza safari usiku saa 5.00 usiku kutoka Bukoba kuelekea mkoani Geita bila kuwa na kibali cha kutoka nje ya mkoa.