Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva bajaji wagoma Simiyu

Bajaji Bariadiii (600 X 350) Dereva bajaji wagoma Simiyu

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHUGHULI za usafirishaji abiria katika mji wa Bariadi, makao makuu ya Mkoa wa Simiyu zimesimama kwa takribani saa moja, mapema asubuhi ya leo kufuatia mgomo wa madreva bajaji uliosababisha na kufungwa kwa barabara kuu ya Bariadi - Shinyanga.

Madereva hao wamefikia uamuzi huo, wakishinikizwa kutekelezwa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambalo alilitoa wakati wa ziara yake mkoani humo mwezi Machi, 2023, ya kuwa magari yote ya abiria makubwa na madogo kuanzia safari zake katika stendi kuu ya Bariadi (Somanda).

Madereva hao wamesema kuwa tangu Waziri Mkuu alipotoa agizo hilo, halijawahi kutekelezwa hali ambayo imewalazimu leo kuamua kufanya mgomo huo wa kufunga barabara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live