Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva ajali iliyoua 13 Songea anaswa akitoroka

AHAJLI TOROKA ER Dereva ajali iliyoua 13 Songea anaswa akitoroka

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takribani wiki moja tangu kutokea kwa ajali iliyoua wafanyabiashara 13 na kujeruhi wengine 12 katika Kijiji cha Namatui wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, Jeshi la Polisi limemkamata Dereva Thobias Njovu (47), akidaiwa kuwa kwenye harakati za kutoroka.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Aprili 9 mwaka huu ambapo, Njovu, mkazi wa Lizabon Manispaa ya Songea akiendesha gari hilo aina ya ya Mitsubishi Fuso lilitumbukia mtoni.

Mara baada ya ajali hiyo, Njovu alitoweka kusikojulikana na jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya aliliambia gazeti hili kuwa wamemkamata.

“Leo (jana) saa nne asubuhi katika stendi ya Super Feo iliyopo Mahenge tumemkamata akijiandaa kutoroka na kwa kuwa tulishasema jeshi la polisi lina mkono mrefu ndivyo ilivyotokea,” alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani Jumatatu kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda huyo aliwataka wananchi kufuata sheria za usalama barabarani na madereva kuzingatia sheria kuepusha ajali zinazoweza kuepukika, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za waharifu ili mkoa uendelee kuwa salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live