Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva afariki ajali Babati

Ajali Kapricon Fds Dereva afariki ajali Babati

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja (Dereva) amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia ajali ya gari (Scania) ambalo liliacha njia na kupinduka katika eneo la Sigino Darajani Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa amesema “Nilisikia kishindo kikubwa na nilifika hapa na kubahatika kumchomoa Mtu mmoja na tayari amepelekwa Hospitali, tulivyoongea nae akasema gari lilikata breki, walikuwa wanne Kwenye gari akiwemo Mwanamke mmoja, eneo hili huwa na ajali nyingi kwasababu kutoka juu kuna mteremko mkali halafu hapa kuna kona"

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema gari lililikuwa na Watu wanne na Dereva ndiye aliyefariki huku majeruhi watatu wakipelekwa katika Hospitali ya Mrara Babati.

"Gari lilikuwa likitoka Kateshi kuelekea Babati wakati wakiteremka Mlima wa Sigino gari hilo liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha Dereva huyo na majeruhi watatu huku chanzo cha ajali ikiwa ni kufeli kwa breki kwa gari hilo"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live